Gharama ya Tabasamu Lake

Jua lilipozama, anga likachorwa kwa rangi za moto na uturi, giza likashuka kama pazia zito na kufunika nchi nzima. Mgao wa umeme uliacha mitaa ya uswahilini ikihema kwa mwanga hafifu wa mbalamwezi kama macho ya paka mwenye kukaribia umauti. Bwana Hoi bin Taaban alikatiza mitaa ya uswahilini akisindikizwa na msongo wa mawazo. Alitembea kama ndege […]